Wanamuziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki na Stamina ambao wanaunda kundi la ‘Rostam’ wanatarajia kuachia albam ya pamoja.

Hayo yamebainishwa na Stamina alipokuwa akiongelea wimbo wao mpya walio upa jina la ‘Watani wa jadi’wimbo ambao ndio wimbo wao wa kwanza kuutoa kama Rostam.

Stamina amewataka mashabiki wa muziki nchini kuwa tayari kwa ujio wa albamu ya wawili hao ambao wameamua kuungana pamoja.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa tayari album hiyo tayari imekamilika na kwa kuanza wataiachia mara baada ya kutoa nyimbo tatu ambazo zitakuwa kama utangulizi na baada ya hapo ndio album itafuata.

Stamina amesema kuwa  muunganiko huo sio kundi bali ni muungano wa family na Roma atabaki kusimama mwenyewe katika kazi zake na yeye atabaki kusimama kama yeye.

Roma na Stamina ni muda sasa wamekuwa wakionekana pamoja mara kadhaa wakifanya’Show’kitu ambacho kimekuwa kikipokelewa vizuri,Stamina kwa sasa anafanya vizuri na kazi iitwayo ‘Love Me’na Roma nae ana kazi mpya inayofanya vizuri inayoitwa‘Zimbabwe.’

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *