Mwanamuziki wa hip hop nchini, Professor Jay kupitia akaunti yake ya Instagram ameeleza kuwa Roma Mkatoliki pamoja na rapper Moni wa Central Zone wamekamatwa na kupelekwa kusikojulikana.

Taarifa hiyo ya Profesa Jay imesema kuwa watu walivamia studio za Tongwe Records jana usiku na kuwachukua wanamuziki hao.

Mbali na wanamuziki hao kuchukuliwa pia wamemchukua kijana wa kazi, computer ya studio pamoja na TV ndani ya studio hiyo.

Kupitia kaunti yake ya Instagram taarifa ya Profesa Jay imesema kuwa”,

ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU… Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana.. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *