Mkali wa Hip Hop nchini, Roma Mkatoliki amesema kuwa hapendezwi na kitendo cha mashabiki kupenda zaidi muziki wa nje kuliko kupenda muziki wa nyumbani.
Roma amesema yeye kama msanii kitu kama hicho kinamuumiza na hajui iwapo ni thamani ya msanii imeshuka hapa nyumbani, au ni kweli muziki wa nje ni mzuri kuliko hapa nyumbani.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa kitendo hiko kinaua muziki wa ndani na kupoteza matumaini ya wasanii wa nyumbani kutokana na mashabiki kupenda zaidi muziki wa nje.
Roma ni mwanamuziki aliyejizolea umaarufu kupitia nyimbo zake zilizofanya vizuri ambapo alikuwa ana ponda sana serikali ya awamu ya nne.