Staa awa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amefunguka kuwa katika maisha yake ya kimuziki, hajawahi kuwa na nidhamu ya uoga kama ambavyo baadhi ya watu wanavyomponda.

Roma alifunguka hayo kufuatia maneno kutoka kwa mashabiki wake kuwa muziki wake utachenji kutokana na hofu, tofauti na alivyozoeleka kuwa na mashairi makali ya kuikosoa serikali.

Roma amesema “Kamwe sijawahi kuwa na nidhamu ya uoga maishani mwangu, kinachotokea kwa sasa ni mabadiliko tu ya muziki wangu, siwezi kuimba siasa kila siku.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa kuimba siasa kila siku zinafanya muziki wangu usiwe wa kimataifa na uwe ni muziki wa ndani,”.

Kauli hiyo ya Roma imekuja baada ya mashabiki wake kusema mkali huyo sasa atakuwa kimya baada ya kutekwa na watu wasiojulikana akiwa studio za Tongwe Records zilizopo masaki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *