Mwanamuziki wa Hip hop, Roma Mkatoliki leo amefundhisha somo la hesabu katika shule ya msingi ya Mchikichini iliyopo Mbagala na kuwapa hamasa wanafunzi kupenda somo hilo na kukabidhi vitabu vya hesabu kwa wanafunzi.

Roma amesema kuwa siku zote muziki wake unagusa maisha ya kila siku ya watu hivyo aliona anapaswa kufanya jambo ambalo litawagusa moja kwa moja na kuamua kwenda shuleni hapo kuwapa hasama wanafunzi hao kupenda somo hilo.

Pia Roma amesema kuwa ameenda shuleni hapo kwa ajili ya kusikiliza kero za shule hiyo ili ziweze kutatuliwa na viongozi mbalimbali hata mashabiki wake wengine.

Roma amesema kuwa “Mimi kama Roma Mkatoliki, kwa kipindi kirefu toka nafanya muziki wangu zaidi ya miaka 10, muziki wangu umekuwa ukiegemea kwenye kuongelea jamii, najivunia sauti yangu inafika mbali, vitu vingi navyozungumza huwa vinafika mbali”.

Roma amemalizia kwa kusema anaamini neno lake linaweza kuwa na nguvu kubwa na kuwafanya wanafunzi hao wakapenda somo hilo na kusema anaamini wapo wasanii wengine wanaweza kuja kufanya jambo jingine kwa wanafunzi hao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *