Mwanamuziki wa hip hop, Roma Mkatoliki amesema kuwa hali yake inaendelea vyema na ameamua kutoka rasmi sehemu aliyokuwepo kwa kufanya misa ya shukrani jana.

Roma Mkatoliki ambaye jana aliambatana na mkewe na kufanya Ibada ya misa takatifu ya shukrani kwa Mungu katika kanisa la St. Peters Oysterbay kumshukuru Mungu kuwavusha katika kipindi kigumu na baada ya hapo Roma amesema sasa anaweza kuendelea na maisha yake ya kawaida.

Msanii huyo amedai kuwa ngoma zake nyingi alizokuwa amezifanya zote zimepotea baada ya vifaa vya studio kuchukuliwa na watekaji.

Roma pia amesema kwa sasa anawaacha Watanzania wawe na shauku hivyo hivyo kutaka kujua akirudi atarudi na ngoma gani.

Mbali na hilo Roma Mkatoliki amesema kwa sasa yupo tayari kufanya show ili maisha yake yaweze kuendelea kama kawaida maana katika kipindi chote yupo ndani hakuna msaada wowote ambao wamepata kutoka kwa viongozi wa serikali.

Roma amesema kuwa  ameamua kuendelea na kazi ili kuendesha maisha yake ya kila siku, huku akiomba kwa yoyote ambaye atagushwa kusaidia studio yao ya Tongwe Records iweze kurudi kama zamani ili waweze kuendelea na kazi zao kama zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *