Mwanamuziki wa hip hop, Roma Mkatoliki jana amefuturisha watoto yatima katika kituo cha Dira kilichopo mitaa ya kwa Mzungu Mbagala Jijini Dar.
Roma amesema aumuzi wa kwenda kufuturu na watoto yatima katika kituo hicho umekuja baada ya kuona ana kila sababu ya Kuungana na watoto yatima na kuwatia moyo katika maisha yao kuelekea kilele ya siku ya watoto duniani.
Amesema kuwa “Tuko katika maadhimisho ya siku ya watoto ulimwenguni, kimisingi nimefurahi kufuturu pamoja na watoto yatima wa kituo hiki.
“Lakini pia nimepata nafasi ya kuwatia moyo na kuzungumza nao mambo mbalimbli kuhusu maisha, watoto pia wamefurahi kuniona na wamepata fursa ya kuniuliza mambo mengi.
“Nimeambiwa kuna changamoto nyingi hapa kituoni, nimewahidi nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha changamoto zile tunazimaliza siku za hivi karibuni kwa kushirikiana na wasanii wenzangu wa hapa nchini”.
Naye mlezi wa kituo hicho Bi Edis Isdori alimshukuru msanii huyo kwa moyo wake kwa kuwateembelea katika kituo chao na kutoa wito kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kurudi katika jamii zao na kushiriki katika mambo mbalimbali.
“Namshukuru Roma mkatoriki kwa kuja na kutufuturisha pamoja na watoto, ukweli ni kwamba watoto wamefurahi na wamefarijika sana.
“Nnitoe wito kwa wasanii wengine wawe na moyo kama wa msanii huyu kwa kuja kwenye jamii na kushiriki pamoja katika mambo mbalimbali.”