Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson amesema wataanza kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano bila ya malipo katika ofisi za kata pamoja na vituo vya afya.

Bi. Hudson amewaambia maafisa wa serikali mkoani Njombe, kwamba mpango huo unadhaminiwa na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumiwa watoto UNICEF, ili kufanikisha zoezi hilo.

Pia Bi Hudson amesema kuwa mpango huo umelenga kuondoa kadhia zinazowakabili wakazi wa vijijini wenye dhamira ya kupata haki hiyo ambapo takwimu zinaonesha maeneo mengi ya vijijini watoto wengi hawana vyeti vya kuzaliwa.

Bi. Emmy Hudson amesema kuwa takwimu zinaonesha ni asilimia nane tu ya watoto wanaozaliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa na kusema kuwa hiyo ni idadi ndogo sana hivyo serikali inapaswa kuongeza juhudi ili watoto wengi zaidi wanapozaliwa wawe na vyeti hivyo.

Kuwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe amewaagiza watendaji wa serikali yake kusimamia zoezi hilo kwa umakini mkubwa ili usilete malalamiko kwa baadhi ya watu kuhusiana na upatikanaji wa vyeti hivyo huku wadau wengine wakichangia kuhusiana na suala hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *