Kamati ya Olimpiki nchini Marekani imethibitisha kwamba waogeleaji wawili wa taifa hilo wamezuiwa kuondoka nchini Brazil.

Baada ya polisi kutilia shaka habari walizotoa kuhusu kushambuliwa na kuporwa mali mjini Rio de Janeiro.

Polisi waliwatoa Gunnar Bentz na Jack Conger kutoka kwa ndege iliyokuwa ikielekea Marekani na kuwahoji.

Waogeleaji hao wawili pamoja na wanamichezo wawili wa kikosi cha Marekani wamesema waliporwa na watu wenye bunduki wakiwa kwenye teksi mjini Rio siku ya Jumapili.

Wanamichezo wenzao, Ryan Lochte na James Feigen pia walizuiwa na jaji kuondoka Brazil.

Lochte tayari ameondoka nchini humo lakini taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema Feigen amezuiwa kusubiri ndege iliyokuwa inaelekea Marekani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *