Aliyekuwa beki wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand ameamua kujikita kwenye masuala ya masumbwi kama mpiganaji.

Hatua ya Rio mwenye umri miaka 38 kujiunga na ndondi imeiungwa mkono na kampuni ya kamari ya Betfair ambayo ilitangaza taraifa hizo leo Jumanne.

Ferdinand amesema kuwa ameamua kujiingiza kwenye ndondi kwa sababu ni changamoto kwake kutokana ameshinda mataji na sasa analenga kushinda mkanda.

Amechapisha video kadha katika mitandao ya kijamii miezi ya hivi karibuni zinazomuanyesha akirusha ngumi na kupata mafunzo.

Aliyekuwa nahodha ya kikosi cha kriketi cha England Andrew Flintoff, pia naye alizindua taalumaa ya ndondi baada ya kustaafu, alipata ushindi mwaka 2012 dhidi ya Mmarekani Richard Dawson kwa pointi.

Ni kampuni ya Betfair iliyomuomba Ferdinand kuanzisha taaluma hiyo na itamsaidia kufuzu na kupata leseni ya bodi ya ndondi ya Uingereza kabla ya kuanza kujifunza na kushindana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *