Brazil imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Olimpiki kwa upande wa mpira wa miguu kwa wanaume baada ya kushinda 6-0 dhidi ya Honduras kwenye nusu fainali ya michuano hiyo jijini Rio.

Mshambuliaji wa timu hiyo Neymar pamoja na Gabriel Jesus kila mmoja ameshinda magoli mawili katika ushindi huo huku magoli mengine yakifungwa na wachezaji Marquinhos na Luan.

Brazil inatarajiwa kukutana na Ujerumani kwenye fainlai hiyo ambapo mabingwa hao wa dunia walishinda 2-0 dhidi ya Nigeria kwenye nusu fainali ambapo magoli yao yalifungwa na wachezaji Lukas Klostermann na Nils Petersen.

Brazil haijawai kutwaa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki baada ya kupoteza fainali tatu za mwaka 1984, 1988 na 2012 jijini London nchini Uingereza.

Fainali hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa Maracana ambapo mashabiki zaidi 78,000 watahudhuria fainali hiyo.

Brazil na Ujerumani walikutana kwenye nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 ambapo Brazil ilifungwa jumla ya goli 7-1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *