Mwanamuziki wa nyota wa Marekani, Rihanna amewapatia baiskeli wasichana nchini Malawi ili kuwasaidia kupata elimu.

Ni mojawapo wa ushirikiano kati ya Wakfu wa mwanamuziki huyo wa Clara Lionel Fountaion na kampuni moja ya baiskli kutoka China Ofo.

Kampeni hiyo kwa jina 1km Action itatoa ufadhili huo ili kuwasaidia mamia ya wasichana kuhudhuria shule za upili nchini malawi.

Wale watakaofuzu kupata ufadhili huo watapewa baiskeli ili kuhakikisha wanakwenda shule kwa usafili huo.

Kulinga na wakfu huo kuna takriban wanafunzi milioni 4.6 nchini malawi lakini ni asilimi nane pekee wanaokamilisha masomo yao ya shule za upili.

Sababu moja ya hali hiyo ni kutokana na ukosefu wa huduma ya uchukuzi nchini humo na kusababisha wasichana kutokwenda shule.

Baada ya kukabidhi baiskeli hizo ”Nina furaha sana kuhusu ushirikiano wa wakfu wa Clara na Ofo kwa sababu utawasaidia wasichana wengi dunini kupata elimu bora”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *