Aliyekuwa makamo wa rais nchini Sudan Kusini, Riek Machar ameruhusiwa kuondoka hospitalini nchini Sudan japo ataendelea kuishi nchini humo kutokana na kundoka Juba wiki iliyopita.

Machar alikuwa akitibiwa mguu wake uliokuwa umevimba kutokana na majeraha iliyopata wakati akitoroka kutoka Sudan Kusini.

Machar anatarajiwa kukutana na rais Omar al-Bashir hivi karibuni kwa ajili ya mazungumzo kutokana na mzozo wa Sudani Kusini.

Machar alifutwa kazi na Rais Kiir kama makamu wa rais baada ya vita kuzuka upya Sudan Kusini.

Wanajeshi watiifu kwake walianza kupigana na wanajeshi watiifu kwa hasimu wake wa kisiasa rais Salva Kiir.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini vilizuka Desemba 2013 kufuatia jaribio la kupindua serikali.

Mapigano yaliendelea hadi kutiwa saini kwa mkataba wa Amani Agosti mwaka jana.

Lakini katika miezi ya hivi karibuni vita vimezuka upya na aliyekuwa makamu wa rais kuambatana na mkataba huo wa amani, Dkt Riek Machar akaondoka mji mkuu Juba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *