Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amekanusha shutuma zilizotolewa dhidi yake kuhusu kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter mbunge huyo amesema kuwa hafanyi biashara hiyo haramu wala hakuwahi kufikiria kuifanya na kwamba nafsi yake ipo tayari kufa masikini kuliko kupata utajiri kupitia njia hiyo.

Pia amesema kuwa anaamini kwamba uchunguzi utafanywa ili kuweza kuweka mambo sawa kwani yeye hana kitu chochote cha kuficha.

Ameongeza kusema kuwa  maneno hayo ya shutuma juu yake ni ya uongo na kwamba yametolewa na watu wasiomtakia mema na wasio na haya.

ridhwani

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *