Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete amempongeza Mama yake baada ya kuteuliwa na Rais Magufili kuwa Mbunge wa viti maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ridhiwan Kikwete amesema kuwa mama Salma Kikwete ni mwanamke wa shoka kwani amewezesha wasichana wengi nchini Tanzania kupata elimu na amekuwa mtetezi wa haki za wanawake hivyo anaamini kupata nafasi ya kuwa Mbunge itakwenda kuwezesha mapambano kuwa sheria rasmi.

Kupitia akaunti yake Instagram Ridhwani ameandika “Umekuwa mtetezi wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia, umewezesha wasichana kupata elimu. Wewe ni mwanamke wa Shoka. Hongera sana kwa uteuzi. Imani sasa umepata sehemu ya kuwezesha mapambano kuwa sheria. Mungu akutangulie Mama yangu , Mheshimiwa Mbunge. Hongera tena”.

riz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *