Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara ya kushtukiza katika Jimbo lake kukaguwa miradi ya kimaendeo.

Katika ziara hiyo amezunguka katika Zahanati na Shule za Secondary Chalize pamoja na mradi wa ufugaji kuku katika Kata ya Msoga ili kuona utendaji kazi wa miradi.

Mh Mbunge Ridhiwani alitembelea katika Hospital ya Msoga ambayo ilijengwa na Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kupitia Ofisi ya Mbunge walitoa vifaa tiba katika Hospital hiyo ikiwamo X-RAY machine, Ado sound Mashine, Vitanda 70,Bed cover, Vitanda zaidi ya 70, mashine za dawa za usingizi zaidi ya tano, mafriji ya kuifadhia damu matatu, kiti kwa ajili ya tiba ya meno na vifaa vingine vingi.

Hospital ya Msoga inatarajiwa kuwa ya wilaya baada ya kukamilisha baadhi ya vitu ikiwemo samani, inaupungufu wa mabenchi ya kukalia wagonjwa 150, viti 150, Meza 40, na Mashelfu ya kuifadhia dawa pamoja na AC katika chumba hicho kwa ajili ya kuifadhia dawa, Ukosefu wa kichomea taka hatarishi pamoja na Mochwari Lakini pia kuna changamoto ya umaliziaji wa chumba cha kuifadhia digital x-ray machine ambayo ni kubwa iliyotolewa na Mh Mbunge

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *