Mwanamuziki nyota wa Marekani, Rick Ross amepunguza bei ya nyuumba yake ya kifahari iliyopo mjini Florida.

Tmz imeripoti kuwa jumba hili kwa sasa litauzwa dola milioni moja na laki tatu ikiwa ni bei ya chini sana ukilinganisha na kiasi alichotoa kununua jumba hilo.

Rick Ross alinunua nyuumba hiyo mwaka 2008 kwa dola milioni $1.25 na akatumia dola laki tano kulirekebisha na sasa anauza jumba hilo.

Rick Ross aliweka nyumba hiyo sokoni kwa bei ya dola milioni $1.5 mwaka 2015 ila sasa ni dola milioni $1.375.

Nyumba hiyo ina vyumba 6 vya kulala, mabafu 5, jiko kubwa, studio mbili za kurekodi,bwawa la kuogelea, jacuzzi.

Hii itakuwa nyumba ya pili Rick Ross ozay kuuza mwaka huu, mwanzoni mwa mwaka huu aliuza nyumba yake nyingine huko Florida kwa bei ya juu na kupokea dola milioni $6.

Staa huyo bado ana nyumba nyingine alilonunua mwaka 2014 kutoka kwa bondia Evander Holyfield kwa bei ya dola milioni $5.8.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *