Mwanamuziki nyota wa hip hop nchini Marekani, Rick Ross amempongeza Diamond Platnumz baada ya jana kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Rick Ross ametoa pongezi zake hizo kupitia akaunti yake ya Facebook ambapo ameweka picha ya Diamond pamoja na kuambatansiha na maeneno ya pongezi kwa mwanamuziki huyo.

Diamond Platnumz hivi karibuni ameonekana katika baadhi ya post za Rick Ross akiwa kama mwakilishi mpya wa pombe ya Belaire kutoka Tanzania, kampuni ambayo Rick Ross pia anafanya kazi kama balozi wa kinywaji hicho.

Hivyo akiwa kama mwanafamilia wa Balaire Rick Ross aliamua kumpongeza msanii Diamond  kwa kazi nzuri anayoifanya  ya kutangaza kinywaji icho vizuri nchini Tanzania.

Katika ukurasa wake wa Facebok Rick Ross aliandika ‘Happy Birthday to my brother Diamond Platinumz ,love how you have been reppin#belaire so with that said, Welcom  to the Belaire Family….#BlackBottleBoy”  aliandiak Rick Ross akiwa ameweka picha ya msanii Diamond katika ukurasa huo.

Daimond jana alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo sherehe yake ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Rency jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *