Mgombea urais kupitia chama cha Republican, Donald Trump amepitishwa na chama hicho kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu nchini Marekani utakaofanyika Novemba mwaka huu.

Trump amepata uungwaji mkono na wajumbe kutoka majimbo na wilaya za Marekani katika kura za mchujo wa kumpata mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama cha Republican kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Cleveland nchini Marekani.

Baada ya kuchaguliwa Donald Trump alitoa shukran zake kwa wananchi kutokana na kumuunga mkono kwenye harakati zake za kuwania kiti cha urais wa Marekani.

Kwa upande mwingine gavana wa jimbo la Indiana nchini Marekani, Mike Pence amechaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Donald Trump kwenye uchaguzi huo.

Trump: Akiwa kwenye moja ya mikutano yake jijini New York.
Trump: Akiwa kwenye moja ya mikutano yake jijini New York.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *