Kiungo wa Ureno na Bayern Munich, Renato Sanches amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi barani Ulaya baada ya kumshinda mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford.
Sanches mwenye umri wa miaka 19 amewafuata nyayo za Wayne Rooney, Raheem Sterling, Lionel Messi na Sergio Aguero katika kushinda tuzo hiyo maarufu kama Golden Boy na hutunukiwa mchezaji bora Ulaya wa chini ya miaka 21.
Rashford na mchezaji wa Bayern Munich, Kingsley Coman walikuwa wanapigania tuzo hiyo na Sanches.
Nyota huyo atakabidhiwa tuzo hiyo katika hafla itakayofanyika Monte Carlo Jumatatu.
Sanches amejiunga na Bayern Munich majira ya joto mwaka huu kwa £27.5m na amewachezea mechi nane msimu huu huku akiichezea Ureno mechi 11.
Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji wa Ureno waliofanikiwa kushinda kombe la mataifa Ulaya mwaka nchini Ufaransa.
Katika mashindano hayo kiungo huyo akiwa na miaka 18 na kuwa mchezaji wa umri mdogo zaidi kuchezea timu hiyo ya Ureno pia alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika michuano hiyo.