Kesho siku ya jumamosi ligi kuu nchini Uingereza inaendelea katika viwanja tofauti nchini humo lakini macho na msikio ya watu yatakuwa katika uwanja wa Old Trafford ambapo Manchester United watakuwa wenyeji wa majirani zao Manchester City kwenye mechi ya ligi kuu.

Mechi hiyo ujulikana kama Manchester Derby ambapo mashabiki wengi wanatarajiwa kuhudhuria katika mchezo huo kutokana na upinzani wa timu hizo.

 Je wajua kama kuna vitu muhimu vya kuvitazama katika kuelekea mchezo huo siku ya kesho jumamosi?

Angalia mambo muhimu kuelekea mchezo huo na uangalia nani anaonekana atashinda mchezo huo.

 1- Vilabu vya Man United na Man City vimewahi kukutana mara 171, wakati Man United wameshinda jumla ya mechi 71 sare 51 na Man City wao wamefanikiwa kuifunga Man United mara 49, hivyo mchezo wa kesho utakuwa wa 172.

 2- Kocha wa Man City Pep Guardiola na kocha wa Man United Jose Mourinho wamewahi kukutana mara 16 wakiwa wanafundisha vilabu vitano, wamewahi kukutana Mourinho akiwa na Real Madrid, Inter Milan na Chelsea wakati Pep alikuwa katika vilabu vya FC Barcelona na FC Bayern Munich hiyo ni katika kipindi cha miaka 7.

 3-Pep Guardiola amemfunga mara nyingi zaidi Jose Mourinho, amewahi kumfunga mara 7 kati ya mechi 16, walizocheza, sare mechi 6 na Mourinho kamfunga Guardiola mara 3 pekee, Guardiola kamfunga Mourinho jumla ya goli 26 wakati Mourinho kamfunga Guardiola goli 16.

 4- Vilabu vya Man United na Man City katika michezo yao 171 waliyokutana wamefungana jumla ya magoli 484, wakati Man United wakiwa wameifunga Man City goli 250 na kuruhusu wao kufungwa magoli 234 tofauti ya goli 16.

 5- Idadi magoli mengi aliwahi kufungwa Jose Mourinho na Pep Guardiola ni goli 5-0 ilikuwa November 9 2010 katika uwanja wa Nou Camp wakati Mourinho ushindi wake mnono aliyowahi kuupata kwa Pep Guardiola ni goli 3-1 akiwa Inter Milan April 20 2010.

6- Cristiano Ronaldo ndio mchezaji wa Man United aliyeoneshwa kadi nyekundu mara nyingi zaidi katika mchezo wa Man United dhidi ya Man City, ameoneshwa kadi nyekundu mara 2.

7- Man United ameshinda jumla ya mechi nne na sare 1 kati ya 5 za mwisho kabla ya kukutana na Man City kesho September 10, katika mechi 5 za Man City wao wameshinda jumla ya mechi zote 5.

8- Mara mwisho timu hizo kukutana katika mchezo wa Ligi Kuu England ilikuwa March 20 2016, mchezo ambao Man United walishinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Marcus Rashford dakika ya 16 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Juan Mata, ushindi ambao waliupata lakini Man City alitawala mchezo kwa asilimia 54 kwa 46.

9- Wayne Rooney ndio mchezaji anayeongoza kwa ufungaji magoli mengi katika durby ya Manchester, amefunga jumla ya goli 11.

10- Jose Mourinho ametwaa jumla ya mataji 22 katika maisha yake ya ukocha, 8 ya Ligi Kuu wakati Pep Guardiola ametwaa mataji 6 ya Ligi Kuu lakini ana jumla ya mataji 21 amwzidiwa taji moja na Jose Mourinho.

Katika mchezo huo wa kesho maafisa wa usalama zaidi ya elfu nne wanatarajia kuwepo uwanjani hapo kwa ajili ya kuhimalisha ulinzi kutokana na mashabiki kuwa wengi na kuzuia fujo kwenye mechi hiyo.

Hiyo ndiyo Manchester Derby usikose kuangalia kwa mara ya kwanza Maourinho na Gurdiola wanakutana katika ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuoneshana ubabe nchini Uhispania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *