Klabu ya Real Madrid imeweka rekodi mpya nchini Uhispania baada ya kucheza mechi 40 bila kufungwa ambapo jana walitoka 3-3 dhidi ya Sevilla kwenye mechi ya Copa del Rey.

Mechi ya mwisho kwa klabu hiyo kufungwa ilikuwa dhidi ya Wolfsburg kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza klabu bingwa ulaya hatua ya robo fainali iliyofanyika nchini Ujerumani Aprili mwaka jana.

Hapo awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Barcelona baada ya kucheza mechi 39 bila ya kufungwa chini ya kocha wao Luis Enrique kati ya mwaka 2015 na 2016.

Sare ya iliyopata Real Madrid dhidi ya Sevilla imeiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Copa del Rey baada ya matokeo ya jumla kuwa 6-3.

Katika mechi hizo 40 Real Madrid imeshinda mechi 31 ikitoka sare michezo 9 tu huku ikishinda magoli 115 na kuruhusu magoli 39 hadi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *