Klabu Real Madrid imetwaa taji la ubingwa wa La Liga baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Malaga na kumaliza ukame wa miaka mitano bila kutwaa kombe hilo.

Madrid ilikua ikihitaji alama moja kabla ya mchezo huo walianza kupata bao la kuongoza katika dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa Cristiano Ronaldo.

Goli la pili limefungwa na mshambuliaji, Karim Benzema akifunga bao la pili katika dakika ya 55 ya mchezo huo.

Madrid wamemaliza msimu wakiwa na alama 93 kwa michezo 38 wakifuatiwa na mahasimu wao Barcelona waliomaliza na alama 90 baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Eibar.

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amekuwa mfungaji bora wa ligi hiyo akimaliza na mabao 37, akifuatiwa na Luis Suarez, mwenye mabao 29, Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya tatu kwa magoli 25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *