Hatimaye miamba ya soka ya Hispania na mabingwa wa ligi ya mabingwa wa Ulaya (Uefa Champions League), Real Madrid wameondolewa kwenye ufalme wa timu tajiri zaidi duniani.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na jarida la Forbes, timu ya mchezo wa mpira wa miguu wa Marekani, Dallas Cowboys.

Hii ni mara ya kwanza kwa Real Madrid kuondolewa kwenye kiti hicho tangu mwaka 2011.

Vinara wapya wa utajiri, Dallas Cowboys wanakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia $4bn (£3.02bn) huku Madrid wakiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia $3.65bn (£2.75bn).

Miamba mingine ya soka barani Ulaya, Barcelona na Manchester United imefanikiwa kuwemo kwenye orodha ya timu 10 tajiri zaidi duniani.

Mabingwa: Wachezaji wa Real Madrid wakisherehekea ubingwa wa Ulaya
Mabingwa: Wachezaji wa Real Madrid wakisherehekea ubingwa wa Ulaya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *