Real Madrid imetwaa kombe la Super Cup baada ya kuilza Barcelona 2-0 katika uwanja wa Bernabeu na kuibuka mshindi kwa jumla ya mabao 5-1.

Mabingwa hao wa Uhispania na Ulaya walitawala mechi hiyo licha ya kutocheza kwa nyota wao Cristiano Madrid.

Marco Asensio ambaye pia alifunga katika ushindi wa mechi ya kwanza huko Barcelona aliwapatia mabingwa hao goli la mapema katika dakika ya nne ya mchezo.

Karim Benzema alifunga goli la pili katika dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo hapa jana.

Real Madrid ilicheza mechi hiyo kwa urahisi mkubwa huku Barca wakifanya mashambulio kupitia Lionel Messi na Suarez yaliogonga mwamba wa goli.

Akiwa kocha wa timu hiyo kwa miaka miwili pekee Zinedine Zidane ameiongoza Real Madrid kushinda mataji mawili ya vilabu bingwa na taji la La liga la 2016-17.

Na kufuatia ushindi huo ni wazi kwamba haitakuwa rahisi kwa timu nyengine kuwabwaga mabingwa hao msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *