Mahakama ya usuluhisho michezoni (CAS) imeipunguzia adhabu ya kutokusajili klabu ya Real Madrid kutoka mwaka 2018 hadi julai 2017..
Kutokana na kupunguzi adhabu hiyo Ream Madrid itaanza kufanya usajili kuanzia Julai mwakani badala ya mwaka 2018 ilivyokuwa hapo awali.
Pia Mahakama hiyo imeipunguzia Real Madrid faini waliyotozwa hapo awali ambapo ilikuwa pauni 282,000 mpaka pauni 188,000.
Hapo awali shirikisho la soka duniani Fifa liliifungia klabu hiyo nchini kusajili wachezaji wapya mpaka mwaka 2018 baada ya kukiuka kanuni za usajili kwa wachezaji chini ya umri wa miaka 18.
Klabu nyingine iliyokumbwa na adhabu ni Atretico Madrid nayo ya Hispani kutosajili baada ya kukiuka kanuni za usajili za shirikisho la soka dunia (FIFA).