Mkuu  wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amewataka watumishi wa umma na wafanyakazi katika sekta zote za uzalishaji kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo kwa taifa.

Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo wakati akitoa salamu za mwaka mpya katika Kanisa la Kirumba Valley Christian Centre (KVCC).

Mongela amesema kumekuwa na mazoea kwa baadhi ya watumishi katika sekta mbalimbali kuona kero wanapotakiwa kufanyakazi kwa makini na uadilifu mkubwa kwa kuwa walizoea kuzembea na kufanyakazi kwa mazoea.

Amesema ofisi yake imeshatangaza mwaka 2017 kuwa mwaka wa kufanyakazi kwa nguvu kubwa.

Amewataka watumishi waliozoea kufanya kazi kwa mazoea kubadilika katika mkoa huo kwa kuwa aina hiyo ya utendaji kazi haishabihiani na serikali iliyopo madarakani lakini pia ni kizuizi cha maendeleo na ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.

Pia amewataka wananchi na waumini wa dini mbalimbali kuendelea kumuombea Rais John Magufuli ili ajenda za maendeleo zifanikiwe katika mwaka huu mpya wa 2017.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *