Mkuu wa mkao wa Mtwara, Halima Dendego amesema kuwa mkoa huo kupata matokeo mabaya kwenye mitihani ya kidato cha pili si jambo la bahati mbaya bali walistahili kutokana na suala la elimu kutopewa kipaumbele mkoani Mtwara.

Dendego amesema kuwa tangu ateuliwe kuongoza mkoa huo, amegundua kuwa mambo mengi hayaendi sawa katika elimu hali iliyomlazimu kujiwekea mikakati ya kujipanga upya.

Aliitaja changamoto nyingine aliyoigundua kuwa ni udanganyifu kwenye mitihani hasa ya kuhitimu elimu ya msingi ambayo watoto wengi hufaulu kwenda sekondari.

mtwara

Amesema Januari 14, aliitisha mkutano wa wadau wa elimu; viongozi wa dini, wa halmashauri na mitaa kujadiliana namna ya kuinua kiwango cha elimu mkoani humo.

Kwa upande wake Ofisa Elimu wa mkoa huo, Fatuma Kilimia alisema amedhamiria kuimarisha usimamizi ili kumaliza tatizo la udanganyifu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *