Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa za kuondoa miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Kilimanjaro Veggies si za kisiasa bali ni taratibu za kisheria za kulinda vyanzo vya maji.

Mghwira alitoa kauli hiyo jana alipotembelea shamba hilo lililopo Kijiji cha Nshara ili kujionea hali ya uharibifu wa mazingira uliofanywa katika shamba hilo linalomilikiwa na Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Mghwira amesema kuwa licha ya mmiliki wa shamba hilo kukubaliana na mkuu wa wilaya kuwa amevunja sheria na angeondoa  mazao yake ifikapo Mei 23 mwaka huu, hakufanya hivyo na badala yake alianza kulima mazao mapya.

Imeelezwa kuwa Mbowe alishawahi kuomba viongozi wa mkoa katika kikao cha RCC kuitishwa kikao ambacho kitajadali masuala ya mazingira na umuhimu wa kuheshimu umuhimu wa mazingira. Kikao hicho kilifanyika lakini RC akasema anashindwa kuelewa kwanini Mbowe ameshindwa kuheshimu.

Akizungumzia uharibifu huo, Mbowe alisema kuwa kwa sasa vijana zaidi ya 100 wamepoteza ajira lakini pia anajadiliana na wanasheria wake kuona nini kinafanyika kutokana na hatua hiyo aliyoiita ya uonevu wa serikali.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *