Jengo la upasuaji kwa wanawake wajawazito limezinduliwa katika Hospitali ya Mwananyamala wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda limejengwa na Taasisi ya isiyo ya kiserikali ya GSM Foundation.

Jengo hilo limepewa jina la Makonda Obstetric Theatre kutokana na yeye kuwa muasisi wa jitihada hizo alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli March 13 Mwaka jana kuwa Mkuu wa Mkoa.

Makonda amewapongeza GSM Foundation na kuwataka watanzania waunge mkono jitihada za wawekezaji wanao wekeza ndani ya nchi, na kuwataka wananchi kununua bidhaa za wazawa kwani mwisho wa siku wanairejesha faida kwa wananchi kwa kufanya miradi ya maendeleo.

Pia amesisitiza suala la ulipaji kodi kwa kila mtanzania serikali yeyote duniani haiwezi kujiendesha bila ya kulipa kodi ndiyo maana Rais Magufuli anasisitiza kulipa kodi, hivyo kila mtanzania ajue anamchango katika maendeleo ya taifa kwa kulipa kodi .

Akitoa Muhtasari wa Mradi Mhandisi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya GSM Foundation waliodhamini ujenzi huo Hersi Saidi ameeleza kuwa ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 420 na kuna vyumba viwili vya upasuaji, huku akisisitiza kuwa watanzania wawe na moyo wa kujitolea kama walivyofanya wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *