Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix J Lyaniva kumaliza tatizo la madarasa 2568 ambayo yanahitajika katika wilaya hiyo baada ya kufanikiwa kutatua changamoto ya madawati.

Makonda amesema hayo katika wilaya hiyo wakati wa muendelezo wa ziara yake ndani ya jiji la Dar es Salaam na kuanisha changamono zinazoikabili wilaya hiyo.

Mkuu wa mkoa anafanya ziara ili kusikiliza changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, Makonda amemtaka DC huyo kutafuta namna ya kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa kwa kutafuta wadau ambao watajenga madarasa hayo kwa utarabitibu wa kuwalipa taratibu.

Makonda ametoa kauli hiyo baada ya mkuu wa wilaya ya Temeke kumtaarifu Mkuu huyo kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa madarasa 2268 ya shule ya msingi na 300 ya shule za sekondari.

Mkuu wa mkoa Paul Makonda anafanya ziara ya siku kumi katika mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya tano za mkoa huo.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *