Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla amewataka watendaji wa vijiji, kata na wataalamu wa halmashauri kufuata taratibu, kanuni na sheria za uhamishaji wa makao makuu ya ofisi za Serikali, ili kupunguza migogoro isiyokuwa ya lazima kwa wananchi.

Makalla amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ilembo Inyara, Shisieta na Insonso, vilivyopo wilayani Mbeya.

Mkuu wa mkoa huyo amesema alilazimika kuyasema hayo baada ya kuibuka kwa mgogoro kati ya wananchi wa Kijiji cha Ilembo Inyara na Shisieta, wanaogombania eneo la kujenga ofisi za kata.

Pia amesema kwamba, ofisi za Serikali hazihamishwi kiholela bali ni lazima zifuate utaratibu hasa zile zinazohamisha makao makuu ya mji kutoka kijiji fulani kwenda kijiji kingine.

“Suala hili limetajwa hata katika Katiba ya nchi na wote lazima tuheshimu Katiba yetu kwani si ya CCM wala Chadema bali ni Katiba ya Tanzania.

Kwa upande mwingine Makalla aliwahakikishia wananchi wa vijiji hivyo kwamba Serikali ya Mkoa wa Mbeya na wilaya, zitaratibu zoezi hilo la uhamishaji wa ofisi ya kata ili haki itendeke na watu wa pande zote waridhike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *