RC Gambo kula sahani moja na wanaoingiza siasa kwenye msiba wa wanafunzi Arusha

0
252

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema serikali itaendelea kuwathibiti watu wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga mbalimbali hasa la vifo vya wanafunzi wa Lucky Vicent.

Gambo amewataka watu kufuata utaratibu na maelekezo yanayotolewa na serikali kwenye suala zima la kutoa rambirambi kwa wafiwa wa msiba wa wanafunzi uliotokea wiki zilizopita.

Mkuu wa mkoa huyo amesema hayo jana wakati anapokea misaada inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali.

Pia Gambo amewataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima.

Mbali na hilo Gambo alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi na amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria, taratibu na maelekezo yanayotolewa na serikali.

Hali hiyo inajiri baada ya wamiliki wa shule binafisi, meya wa Arusha pamoja na waandishi wa habari kukamatwa na jeshi la Polisi mkoani Arusha baada ya kupeleka rambirambi baada ya kupitia kwa mkuu mkoa.

LEAVE A REPLY