Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amezindua daraja la mto Kijenge linalounganisha kata za Engutoto na Moshono ambalo limejengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Dharam Singh Hanspaul.

Akizungumza katika uzinduzi huo mkuu wa mkoa amesema ni ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikuwa wakipata hadha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika.

Daraja: Muonekano wa daraja la Kijenge baada ya kukamilika.
Daraja: Muonekano wa daraja la mto Kijenge baada ya kukamilika.

Pia katika uzinduzi wa daraja hili mkuu wa mkoa alitumia fursa kusikiliza kero za wananchi walioudhuria ambao wamelalamika uuzwaji holela wa maeneo ya wazi ya Serikali yanayofanywa mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *