Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa hakuna mtumishi wa serikali au mtu yoyote ambaye anaweza kuvumiliwa kama atakuwa amelenga kuikwamisha serikali katika jambo lolote lile.

Mrisho Gambo amesema hayo alipokuwa akiongea na watumishi wa serikali Mkoa wa Arusha.

Ameema ameona watumishi wengi wamekuwa wakisuasua kwenye utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli ambalo linataka kila mkoa na kila Wilaya kuhakikisha wanajenga viwanda ili kufikia Tanzania ya viwanda ambapo mpaka sasa kwa Mkoa wa Arusha hakuna kiwanda hata kimoja ambacho kimejengwa.

Lakini mbali na hilo Mkuu wa Mkoa aliwakumbusha wafanyakazi hao kuhusu agizo la Rais Magufuli kuhusu ujenzi wa viwanda

Kwa mujibu wa Rais Magufuli mpaka sasa mkoa ambao umeongoza kwa kutekeleza sera ya viwanda ni Pwani.

Rais Magufuli akiwa ziarani Pwani aliutangaza mkoa huo kuwa ndiyo mkoa wa viwanda Tanzania kwani wameshaanza kutekeleza kwa kujenga viwanda, ambapo mpaka sasa mkoa huo unakadiriwa kuwa na zaidi ya viwanda 300 vikubwa na vidogo dogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *