Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameigiza TAKUKURU mkoani humo kuhakikisha inawakamata na kuwafikisha mahakamani wale wote waliokula fedha shilingi 448.9 za mradi wa machinjio katika shamba la Manyara ranch.

Gambo amesema hayo baada ya kutembelea machinjio hayo yaliyopo katika shamba la Manyara ranch na kusema kuwa mradi huo ulianza mwaka 2009 hadi haujamalizika.

Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa fedha zimetolewa na wafadhiri wa USAID kupitia Shirika African Wildlife Foundation (AWF) lakini fedha zote zimeliwa na mradi umekwama kuendelea hadi sasa.

Gambo ameendelea kusema kuwa TAKUKURU inapaswa kuchukua hatua na kuwasaka wale wote waliohusika kuhujumu mradi huo kwa kutafuna fedha za mradi mpaka kupelekea mradi kukwama kwa hiyo lazima wawajibike kwa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *