Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ametaja kolabo zake na wasanii wa nje ambazo zipo tayari kwasasa.

Rayvanny amesema kuwa tayari ameshafanya kolabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.

Mwanamuziki amesema kuwa “Nina kolabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria, ingawa kwa sasa siwezi kutaja jina lake.

Lakini pia kuna kolabo Afrika Kusini, na Kenya ukiacha Bahati, kuna mwingine Khaligraph Jones kutoka Nairobi.

Kwa msanii wa Afrika Kusini tayari muimbaji huyo kutoka WCB ameshafanya kolabo na Dj Maphorisa tangu mwezi Disemba mwaka jana inasubiliwa muda tu kuachia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *