Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva Raymond ‘Rayvanny’ kutoka WCB amesema kuwa  EATV AWARDS zitaongeza hamasa ya kufanya juhudi kwenye sanaa yake kama msanii anayechipukia kwasasa.

 Raymond amesema yeye kama msanii chipukizi kwanza amezifurahia tuzo hizo kwani zina mchango mkubwa sana, ikiwemo kuongeza juhudi zaidi ili aweze kuishinda na kujiwekea misingi mizuri ya sana yake.

Rayvanny amesema kuwa “Nilifurahi kwa sababu inakuwa inaonesha picha nzima ya muziki jinsi unavyokwenda, mtu akiona jamaa kachukua tuzo na mimi nifanye juhudi na mimi nichukue, nimefurahi sana uwepo wa tuzo ni kitu kizuri kinaonesha thamani ya muziki wetu”,.

Utoaji wa tuzo hizo utafanyika katika ukumbi wa Mlima City ifikapo Disemba 10 mwaka huu.

Tuzo hizo zinahusisha wasanii wa filamu na muziki kwa nchi za Afrika Mashariki, na pia ndizo tuzo kubwa za kwanza kuanzishwa Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *