Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny aliyeshinda tuzo ya BET kipengele cha International Viewers Act 2017 amewasili nchini leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)

Rayvanny alipata tuzo hiyo nchini Marekani Juni 25 na kuwa msanii wa kwanza kutokana Tanzania kushinda tuzo hizo kubwa.

Rayvanny ameambatana na Babutale ambaye ni mmoja wa mameneja wa Kundi la WCBlinaloongozwa na Diamond.

Meneja wake, Makame Fumbwe amesema kuwa Rayvanny atakapowasili, msafara wake utatoka JNIA na kupita katika mitaa mbalimbali ya jiji na baadaye atakwenda katika mahojiano kwenye kituo cha Clouds.

Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza licha ya kumpongeza kwa mafanikio hayo lakini amesema Rayvanny hakutoa taarifa kwa baraza kuwa anakwenda kwenye tukio hilo kubwa akiliwakilisha taifa.

Amesema ni ngumu kwa baraza kumpatia mapokezi kwa kuwa hawana taarifa rasmi za ujio huo na hata alipoondoka hakuaga.

Mngereza amewataka wasanii wote nchini kuwa karibu na chombo hicho kwani kimeundwa maalum kwa ajili yao hivyo ni muhimu wanapokwenda nje ya nchi kwa ajili ya programu zozote za kuliwakilisha taifa wawe wanaaga na kutoa taarifa.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *