Staa wa Bongo fleva, Raymond amesema kwamba sababu kubwa ya kuchelewa kwa video ya wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ ni kutokana na baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo huo kushindwa kuonesha ushirikiano.

Raymond amesema baadhi ya wasanii aliowataja kwenye wimbo wake ‘Natafuta Kiki’ wamekuwa wagumu kupatikana na ndiyo mana hadi sasa hivi video ya wimbo huo bado haijatoka.

Staa huyo ameongeza kwa kusema menejimenti yake ya “WCB” ilimleta director kutoka nje ya nchi ili kushoot video ya wimbo huo lakini baada ya wasanii kushindwa kuonesha ushirikiano wakamruhusu kurudi kwao kwanza baada ya hapo atakuja tena kwa ajili ya video hiyo.

Kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kuiona video ya wimbo huo, Raymond ameachia video ya wimbo huo ikiwa ni Guitar Version kwa ajili ya mashabiki wake.

Raymond ameweka wazi kwamba video hiyo itafanyika lakini hajataja itachukuwa muda gani kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *