Muigizaji wa Bongo Movie, Vicent Kigosi (Ray) ametoa ya moyoni kuhusu serikali kuwasahau wasanii licha ya kufanya kampeni.

Ray amesema kuwa wasanii waljitolea sana kwenye kampeni mpaka kulala sehemu siziso na hadhi zao ili kuhakikisha viongozi hao wanaingia madarakani lakini viongozi hao wamewasahau wasanii.

Muigizaji huyo amesema kuwa kazi walioifanya siyo ndogo kutokana na kampeni za mwaka 2015 zilikuwa ngumu kutokana na upinzani mkubwa uliokuwepo katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Pia amesema kuwa kampeni hizo zimesababisha wapoteze mashabiki wao wengine kutokana na wao kupiga kampeni za CCM na kuwapoteza mashabiki wao ambao walikuwa chama pinzani.

Ray amewataka viongozi hao kuwakumbuka wasanii hao kutokana na mchango wao wakati wa kampeni za uchaguzi uliosababisha waingine madarakani.

‘Serikali inatakiwa kuwaangalia hawa wasanii kwasababu wamepambana sana mpaka wao waingie madarakani’ Amesema Ray.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *