Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Ray C amesema kuwa wakati alipokuwa anatumia madawa ya kulevya ailkuwa kwenye wakati mgumu sana lakini anamshukuru mungu kwa kumtoa kwenye janga hilo.

Ray C amekema kuwa yeye alishakufa ila anamshukuru Mungu kwa wema wake na kumtoa katika janga hilo la dawa za kulevya.

Ray amesema kuwa kwasasa anasimama mstari wa mbele kama muhanga wa dawa za kulevya kupinga vita dhidi ya dawa hizo kwani zimepoteza maisha ya vijana wengi na kuharibu ndoto za watu.

 Pia Ray C anasema muathirika wa dawa za kulevya kumpeleka jela halimsaidii chochote hivyo ameiomba serikali kufungua vituo vya ‘Rehabilitation’ kwani anasema matumizi ya methadone hayasaidii kitu kwani zile nazo ni dawa za kulevya tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *