Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ray C ameunga mkono harakati zinazofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Slaama, Paul Makonda kuhusu suala la madawa ya kulevya.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Ray C ameposti video ikimuonesha mwanamke aliyepoteza maisha kutokana na matumzi ya madawa ya kulevya ambapo ni janga la dunia kwasasa.

Kwenye video hiyo Ray C ameandika maneno yanayosema ‘SAY NO TO DRUGS’ akionesha hasira zake kuhusu madawa ya kulevya yanayouwa nguvu kazi ya taifa kutokana  na matumizi hayo.

Ray ambaye alikuwa akitumia madawa hayo ambapo alipewa huduma katika vituo mbali mbali ‘Sober House’ mpaka kupeleka kupona kwa sasa na kurudi katika hali yake ya kawaida licha ya mwili wake kudhoofika.

Ray C amewahamasisha watu wengi kupitia video aliyoiweka katika mtandao na imewagusa Watanzania wengi kwa kuchangia maoni yao juu ya athari mbaya za madawa ya kuleva na sakata la linalonguruma kwa sasa nchini.

Hivi karibu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwataja wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie wanaohusika na uuzaji wa madawa ya kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *