Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva Rehema Chalamila ‘Ray C’ amemjia juu msanii mwenzake Nandy baada ya kutumia nyimbo zake bila ruhusa.

Ray c alionekana kukasirishwa na kitendo cha Nandy kutumia nyimbo zake kwenye tamasha linaloendelea la Fiesta licha ya yeye kutokualikwa kushiriki tamasha hilo. .

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray C alimfungukia Nandy yafuatayo:

Jamani hii tabia sio nzuri kabisaa! Sijafa bado!  Kama mnaona umuhimu wa sauti yangu kwenye shoo zenu muwe mnaniitaga basi! Sina Kansa ya koo ya kushindwa kuziimba hizo nyimbo Nandy hii ni Mara ya mwisho ukipanda Fanya kazi zako! Hii ni mara ya pili ujue, Mashabiki zangu hamuwatendei haki ujue! I don’t like it sipendi, Maana hata tukigongana salamu saa nyingine hamna kwaiyo sitaki mazoea! Niliimba tusitafutiane visa tena pisha sio tena presha, sitaki unafki na wewe Tena, mna nini lakini? Kila mtu apate riziki kwa jasho lake”.

Baada ya kuona povu la Ray c na mashabiki kumjia juu Nandy kwa kitendo alichofanya Nandy aliomba radhi;

Dada angu Ray c, kama wote tulivyosema kabla ya kuimba juzi, mimi ni mmoja wa wasanii wanaokukubali kama msanii uliyetufungulia njia ya mziki wetu ulipo, sitaacha kukuheshimu na kukukubali  kwa hilo  wewe na wengine wengi tu. Siamini kukusifia na kukuenzi ni lazima uwe umekufa hapana nafanya jambo hili zuri kwa moyo wangu mzuri Kama ulivyomuenzi Mama mwanahela kwa nyimbo zake. Heshima yangu kimuziki kwako itabaki siku zote kama nilivyoimba nyimbo za wasanii Kama king kiki, mwasiti, Yemi Alade na Recho”.

Ray C alionekana kukerwa na kitendo cha Nandy kulipwa kushiriki tamasha la fiesta na kutumia nyimbo zake wakati yeye mwenye nyimbo hajalipwa kushiriki tamasha hata moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *