Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Lady Jay Dee amesema kuwa ratiba zinasababisha kutofanya nyimbo na Diamond Platnumz lakini yupo tayari kufanya nae nyimbo muda wowote watakapokuwa tayari.

Kauli hiyo ya Jay Dee imekuja kufuatia kuongezeka kwa minong’ono miongoni mwa mashabiki wa muziki huo kuwa wawili hao wanakwepana na hawataki kufanya nyimbo pamoja.

Jay amesema hana tatizo na msanii yoyote nchini na yuko wazi wakati wowote kwa muda ukifika atafanya nyimbo na Diamond japokuwa akusema lini atafanya nyimbo na mkali huyo kutokea WCB.

Ikumbukwe kuwa wwezi Novemba mwaka jana, Diamond alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema yuko tayari kufanya kazi na mwanadada huyo lakini tatizo ni kubanwa na ratiba ambayo imekuwa haimpi nafasi.

Kutokana na kauli za wanamuziki hao sasa ni dhahiri hawana shida kufanya kazi pamoja lakini huenda wanaogopana huku kila mmoja akisubiri mwenzake amuanze, maana hadi sasa hakuna ambaye ameomba kufanya kazi na mwezake huku wote wawili wakidai kukwamishwa na ratiba ya kazi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *