Ligi Kuu soka Tanzania Bara mzunguko wa 15 unaendelea tena leo kwa michezo minne katika viwanja tofauti.

African Lyon inatarajiwa kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Mbao FC itakuwa mwenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ndanda FC watakuwa mwenyeji wa Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Tanzania Prisons inatarajiwa kuialika Yanga kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Kagera Sugar itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba huku JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

Ligi hiyo itaendelea tena Jumatatu kwa michezo miwili ambako Mtibwa Sugar itaialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Manungu uliopo mkoani Morogoro wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *