Ligi Kuu Tanzania Bara maarufu kama VPL inatarajia kuendelea leo Jumatano pamoja na kesho Alhamisi kwa mchezo mmoja.

Ruvu Shooting ya Pwani ambayo itaikaribisha Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Mabatini uliuoko Mlandizi mkoani Pwani.

Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Morogoro utafanyika katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamanzi.

Ndanda FC  dhidi ya Mbeya City  kwenye mechi itakayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Prisons ya Mbeya na Stand United itakayokuwa mgeni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya

 Toto African ya Mwanza itaikaribisha Yanag kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

African Lyon itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho Alhamisi Oktoba 20, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambako vinara wa ligi hiyo kwenye msimamo hadi sasa, Simba itakuwa mwenyeji wa Mbao FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *