Klabu ya Yanga imethibitisha kuachana na kiungo wao Haruna Niyonzima baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kuendelea kuchezea klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake mwezi julai mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa Katibu Mkuu, Boniface Mkwasa kwa kusema hawataweza kuendelea na Niyonzima katika msimu ujao wa 2017/2018 baada ya kumaliza mkataba wake mwezi Julai.

Mkwasa amesema kuwa “Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga SC, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo, Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla”.

Niyonzima mbaye alichezea misimu sita mfululizo kwa kiwango cha juu bado haijawekwa wazi ni wapi anaelekea baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga SC.

Kiungo uhenda akaamia klabu ya Simba baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwezi Julai mwaka huu kutokana na timu hiyo Msimbazi kuonesha nia ya kumsajili.

Niyonzima kwasasa yupo kwao nchini Rwanda kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi nchini Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *