Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ametangaza rasmi kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania.

Pia amesema kuwa Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.

Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.

Kwa upande wa Mama yake Wema pia amerudisha kadi ya CCM kusema huku akisema tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *