Klabu ya Everton imekamilisha usajili wa kiungo, Morgan Schneiderlin kutoka Manchester United kwa ada ya uhamisho iliyogharimu paundi milioni 24.

Kiungo huyo raia wa Ufaransa amesaini mkataba wa miaka minne ambapo mkataba wake utamuweka Goodson Park mpaka msimu wa mwaka 2021 baada ya kufuvu vipimo vya Afya ndani ya klabu hiyo.

shesn

Schneiderlin lijiunga na Manchester United akitokea klabu ya Southampton baada ya kusajili wa kwa ada ya uhamisho paundi milioni 25 chini ya kocha Louis Van Gall msimu wa mwaka 2015.

Mchezaji huyo ameamua kuondoka Manchester United baada ya kukosa namba chini ya kocha Jose Mourinho ambapo amecheza mechi tatu tu za ligi kuu msimu huu.

Kiungo huyo anaungana na kocha wake wa zamani Ronald Koeman ambaye alimfundisha kipindi alipokuwa Southampton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *